Sunday, December 4, 2011

Aanika nyeti zake ili kuonesha uhuru wa kujieleza

Katika vituko vya dunia ya leo, Alia Al-Mahdy Msichana wa kimisri ameanika picha yake ya utupu/uchi wa mnyama katika mtandao wake wa Twitter ili kuonesha namna anavyopigania uhuru wa kujieleza.

Msichana huyo ametetea kitendo chake hicho kwa kusema kuwa huo ni uhuru wa kujieleza. Demu huyo ni mmoja wa waandamanaji waliomng`oa rais wa zamani wa Misri Hosni Mubaarak.

Hata hivyo tukio lake limesababisha gumzo kubwa miongoni mwa wamisri. Wafuasi wa mlengo wa kiliberali wanaona kuwa kitendo hicho kitawapakazia na kuwaharibia mbele ya raia wengine ambao hawapendi vitendo kama hivyo.

Kwa upande mwingine raia wa Misri, Wakristo kwa Waislamu wamelaani kitendo hicho. Vilevile, msichana huyo alikumbana na wakati mgumu sana alipoenda tena eneo la kiwanja cha Tahriri ili kujumuika na waandamanaji wanaodai jeshi liachie madaraka haraka. Waandamanaji hao walimfukuza bila kumpa uhuru wa kujieleza alioutaka kwa kuanika nyeti zake


Source: nifahamishe.com

No comments:

Post a Comment